Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa amezindua shamba la bangi kwa ajili ya dawa lenye thamani ya dola za kimarekani milioni 27.

Shamba hilo limewekewa kiwanda cha kisasa cha usindikaji ambacho bangi yake itatumika kama suluhisho la matibabu ya kibaolojia na bidhaa za dawa katika soko la ndani na la kimataifa.

Mradi huu ni kwa ushirikiano na Serikali ya Uswizi kupitia kiwanda cha Swiss Bioceuticals na Serikali ya Zimbabwe.

Rais Mnagangwa amesema kuwa ushirikiano huo unaonyesha imani ya Uswizi katika kuwekeza ndani ya uchumi wa Zimbabwe huku akisema kuwa taifa hilo la Ulaya tayari limeshirikiana na Zimbambwe katika miradi mingine kama vile viwanda, usindikaji wa chakula na ujenzi wa taasisi mbalimbali.

RC Kagaigai awataka wazazi kuwafundisha wato wao upendo
Palestina yaunga mkono uchunguzi wa kimataifa kwa kifo cha mwandishi