Rais wa Nigeria, Muhammadu Buhari amesema kuwa anaangalia uwezekano wa kushirikiana na raisi wa Ghana kupambana na tatizo la rushwa.

Amesema kuwa ni muhimu kwa viongozi sahihi kuhakikisha wanapunguza umasikini Barani Afrika na kuzingatia ustawi wa demnokrasia.

Ameyasema hayo jana kwenye sherehe za kutimiza miaka 61 Uhuru wa Ghana ambapo ameunga mkono jitihada za raisi wa nchi hiyo, Nana Akufo-Addo za kupambana na rushwa.

“Naipongeza Serikli na bunge kwa kupitisha haraka muswada wa kuwa na muendesha mashtaka mkuu na kusainiwa kuwa sheria,’’amesema Rais Buhari.

Aidha, Muendesha mashtaka mkuu, Martin Amidu ameanza kazi mapema wiki hii baada ya kuthibitishwa na kamati ya bunge wiki mbili zilizo pita na anategemewa kuongoza kampeni ya Serikali dhidi ya mapambano ya rushwa.

Hata hivyo, Rais Buhari ameongeza kuwa jitihada zinazofanywa na serikali ya Ghana kupambana na rushwa zitasaidia nchi hiyo kupata wawekezaji wengi kutoka nje.

Nape awataka wabunge kuunga mkono hoja ya Bashe
Kampuni ya Coca-Cola kutengeneza kinywaji chenye kilevi