Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli amempandisha cheo na kumteua, Mohamed Hassan Haji kuwa Kamishna wa Polisi Zanzibar.

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, John Kijazi imesema kuwa, Rais Dkt. Magufuli amempandisha cheo Mohamed Hassan Haji kutoka Kamishna Msaidizi (ACP) na kuwa Kamishna wa Polisi (CP) na kisha kumteua kuwa Kamishna wa Zanzibar.

Aidha, Kabla ya uteuzi huo Kamishna wa Polisi Zanzibar, Mohamed Haji alikuwa mhasibu mkuu wa jeshi la Polisi Zanzibar.

Hata hivyo, Kamishna Haji anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Kamishna wa Polisi (CP) Hamad Omar Makame ambaye amestaafu.

Kim Jong un amualika Rais wa Korea Kusini
Video: Kibao kingine cha Mbosso chini ya WCB ''Nimekuzoea''