Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Dkt. John Magufuli amesema kuwa chama hicho hakitambembeleza mtu kukichangia katika shughuli mbalimbali.
Ameyasema hayo wakati akihutubia Mkutano Mkuu wa CCM uliofanyika mjini Dodoma, Dkt. Magufuli amesema kuwa miaka yote CCM imekuwa ikiomba omba hata kwa watu ambao hawastahili.
“Chama chetu kimekuwa omba omba, matokeo yake watu wamekuwa wakitumia nafasi hiyo kudhalilisha. hakuna tena omba omba hatutaki kumbembeleza mtu akitaka kutuchangia atuchangie,”amesema Rais Dkt Magufuli.
Hata hivyo, Rais Magufuli amesema kuwa chama hicho kina utajiri ambao unakiwezesha kujitegemea na kwamba mwanachama atakayetumia mali za chama hicho kwa maslahi binafsi atachukuliwa hatua kali

Malawi Yazikacha AFCON, CHAN
Magazeti ya Tanzania leo Machi 13, 2017