Rais wa shirikisho la soka nchini Italia (FIGC) Gabriele Gravina, amesema msimu wa Serie A unaweza kufika hadi Oktoba ili kuzuia malalamiko.

Serie A imesimamishwa tangu mwezi Machi 9, kutokana na janga la Corona, ambapo kesi zaidi ya watu 15,000 wamefariki kutokana na virusi hivyo nchini humo.

Baadhi ya viongozi wa ngazi za juu wa klabu zinzoshiriki ligi ya Serie A, walipendekeza kwamba msimu unapaswa kufutwa, huku Lazio na Juventus wao ndio wapiganie ubingwa Scudetto.

Lakini Rais wa FIGC, anaamini msimu lazima umalizike, hata ikiwa utaingia kwenye msimu wa  2020/2021, na wanahofia kwamba wanaweza kukumbana na changamoto za kisheria ikiwa hawatafanya hivyo.

Mgogoro mkubwa unatajwa kuweza kutokea kwa timu zinazowania kushiriki michuano ya Ulaya, na zile zinazopambana kutoshuka daraja.

Corona yamlaza ICU Waziri Mkuu Uingereza, amtaja wakumsaidia kazi
Rais Kenyatta: Namuombea 'kigogo' aliyekwepa karantini afungwe miaka 10 jela