Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania awamu ya Tano Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Prof. Idris Suleiman Kikula kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Madini.

Taarifa hii imetolewa na Katibu Mkuu kiongozi Balozi, John Kijazi na amesema uteuzi huu umeanza kuanzia tarehe 17, Aprili 2018.

Aidha Rais, amewateua Makamishna wa Tume ya Madini kama ifuatavyo;

  1. Doto James kuwa Katibu Mkuu Fedha na Mipango
  2. Dorothy Mwanyika kuwa Katibu Mkuu Ardhi na Maendeleo ya Makazi.
  3. Florens Turuka kuwa Katibu Mkuu Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT)
  4. Mhandisi Musa Iyombe kuwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)
  5. Haroun Athuman  Kinega  kuwa Mtendaji Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wachimbaji wadogo wa Madini
  6. Evaristo Emmanuel Lungopa kuwa Naibu Mwanasheria wa Taasisi ya Jiolojia na Utafutaji Madini (FEMETA)
  7. Athanas Simon Macheyeke kuwa Katibu Mtendaji wa Taasisi ya Uhamasishaji, Uwazi na Uwajibikaji katika Maliasili za Madini, Mafuta na Gesi Asilia (TEITI)

Wakati huohuo Rais Magufuli amemteua Balozi Mstaafu Daniel Ole Njoolay kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mpango wa kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA).

 

 

Video: Polepole amlipua Zitto, amtaka aache kudanganya umma
Auawa kisa wivu wa mapenzi