Leo Septemba 5, 2018 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli amefanya ziara na kutembelea shule ya msingi Mwisenge aliyosoma Hayati Mwalimu Julias Kambarage Nyerere na kuwaahidi kuwapatia kiasi cha fedha Milioni 2o ndani ya wiki mbili na kutaka fedha hizo zitumike kukarabati shule hiyo.

Mbali na ahadi hiyo Rais Magufuli ametoa papo kwa papo kiasi cha fedha Shilingi Milioni Moja kwa wanafunzi wenye ulemavu wa ngozi pamoja na macho ili washerekee fedha hiyo na walimu wao.

Aidha Rais amewataka wanafunzi hao wasome kwa bidii kwani Serikali inawawependa na kuwajali.

Siri ya Laurent Koscielny kuikacha Arsenal yafichuka
Video: Ona Rais huyu anavyolindwa vikali, sababu zatajwa

Comments

comments