Mgombea urais atakayepeperusha bendera ya chama cha Rais wa Jamhuri ya Demokrasia ya Congo Joseph Kabila katika uchaguzi mkuu nchini humo unaotarajiwa kufanyika Desemba mwaka huu atatangazwa leo Jumatano kwa mujibu wa msemaji wa rais.

Wanachama wa muungano wa vyama vya Common Front for Congo (FCC) waliitwa kwenda kwenye jumba la kifahari la rais Kabila nje kidogo ya mji wa Kinshasa jana Jumanne kwa ajili ya kupanga mikakati muhimu.

Aidha, baada ya mazungumzo hayo hapo jana, msemaji wa Kabila Lambert Mende, aliwaambia waandishi wa habari kuwa mgombea atajulikana mapema asubuhi ya leo.

Rais Kabila amekuwa madarakani tangu mwaka 2001 na alikataa kuondoka mwishoni mwa mwaka 2016 wakati mihula yake miwili ya kikatiba ilipokamilika lakini bado amekataa kusema kama atawania tena kiti hicho.

Hata hivyo, Wagombea ambao tayari wametangaza kuwa watawania urais ni Jean-Pierre Bemba, Felix Tshisekedi, kiongozi wa chama cha Union for Democracy and Social Progress (UDPS), Tryphon Kin-Kiey Mulumba aliyekuwa msemaji wa Mobutu Sese Seko ambaye ni mgombea huru, huku Moise Katumbi akizuiliwa kuingia nchini humo.

Ethiopia yatia saini mkataba wa amani na kundi la OLF
Steve Bruce kuamua hatma ya Jack Grealish