Rais wa Jamhuri ya Rwanda na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Paul Kagame anatarajia kuwasili nchini tarehe 7 Machi 2019 kwa ziara ya kikazi ya siku mbili., ziara hiyo inafanyika kufuatia mwaliko wa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Ziara hiyo itatoa fursa kwa viongozi hao wawili kujadiliana masuala mbalimbali kuhusu uhusiano na ushirikiano baina ya nchi hizi mbili na wanatarajia kuzungumzia masuala mbalimbali ya mtangamano katika Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Rais wa Jamhuri ya Rwanda, atawasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere saa Tisa Alasiri tarehe 7 Machi 2019 na kupokelewa na mwenyeji wake, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

 

Siza wa Clouds FM asimulia kilichompata Kibonde kabla ya kupoteza maisha
Video: Katoliki watoa waraka mzito, Hukumu ya kifo.

Comments

comments