Rais wa Shirikisho la  soka nchini (TFF), Wallace Karia ameunda Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom  Tanzania Bara msimu wa 2017/18.

Kamati hiyo itaongozwa na Mwenyekiti Ahmed Mgoyi wakati Makamu Mwenyekiti ni Almas Kasongo ilihali  Amiri Mhando ameteuliwa kuwa Katibu wa kamati hiyo ya tuzo.

Mhando ni Mhariri wa Gazeti la Spotileo linalotolewa na Kampuni ya Magazeti ya Serikali – Tanzania Standard Newspaper (TSN).

Wajumbe ambao wameteuliwa ni Ibrahim Kaude; Mkuu wa Kitengo cha Michezo katika Kampuni ya Azam Media, Patrick Kahemele na Kocha mkongwe wa soka, Kenny ‘Mzazi’ Mwaisabula.

Kadhaika Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya Uchapishaji ya Global (Global Publisher inayochapisha magazeti kadhaa likiwamo Championi), Saleh Ally; Mtangazaji mahiri wa michezo kutoka Kituo cha Redio cha EFM, Ibrahim Masoud na Mtangazaji wa Vipindi katika Kituo cha Radio ya Watu, Fatma Likwata.

Pia wapo waandishi Mwandamizi wa Michezo wa Gazeti la Mwanaspoti linalochapishwa na Kampuni ya Mwananchi Communication (MCL), Gift Macha, Mhariri wa Michezo wa Gazeti la HabariLeo linalotolewa na TSN, Zena Chande.na Katibu Mkuu wa Chama cha Wachezaji wa Mpira wa Miguu, Said George.

Viingilio mchezo wa Azam FC v Simba SC
Matokeo ya usaili kwa wanaogombea TPLB