Mahakama nchini Kenya imempatia siku 14 Rais wa nchi hiyo Uhuru Kenyatta kuwateua majaji sita waliosalia kati ya wale 40 , katika kipindi cha siku 14 zijazo,

Majaji hao sita wanashirikisha Aggrey Muchelule, George Odunga, Weldon Korir na Joel Ngugi, ambao walifaa kuhudumu katika mahakama ya rufaa.

Hakimu mkuu Evans Makori na msajili wa mahakama kuu Judith Omenge pia waliachwa nje katika orodha ya majaji waliochapishwa katika gazeti la Kenya.

Siku ya Alhamisi , Jaji wa mahakama kuu William Musyoka , James Wakiaga na George Dulu walisema kwamba Jaji mkuu Martha Koome, pamoja na tume ya mahakama watakuwa huru kuwaapisha majaji hao sita iwapo Rais Uhuru Kenyatta atashindwa kutekeleza jukumu lake la kikatiba.

‘’Siku 14 zitakapokamilika, bila uhuru kutangaza uteuzi huo, itabainika kwa uwezo wake wa kuwateuwa utakuwa umekwisha na hivyobasi sita hao watakuwa wameteuliwa kama majaji wa mahakama ya rufaa kama ilivyopendekezwa’’, walisema majaji hao.

Majadiliano mkataba wa Nchi hodhi yanukia
Habari kubwa kwenye magazeti leo, Oktoba 22, 2021