Rais Uhuru Kenyata jana aliungana na marafiki wa Raila Odinga kusherekea siku ya kuzaliwa ya Odinga ambapo alionekana ameketi kwenye meza moja na Raila na marafiki wengine huku gumzo ikionekana kunoga kati yao.

Ijumaa Januari 7 ilikuwa ni siku ya kusherekea siku ya kuzaliwa ya Raila huku akitimia miaka 77. Raila aliungana na wafuasi wake kwenye ukumbi wa Bomas ambapo alikata keki na kufurahia afya aliyotunukiwa na Muumba.

Baadaye, ‘Wakuu hao’ walikuwa wameandaa sherehe nyingine ambapo wafanyabiashara wakubwa nchini Kenya na vigogo wa kisiasa walihudhuria.

Hata hivyo duru za kisiasa nchini Kenya zinasema kuwa Rais Kenyata amekuwa akionekana kumpendelea Raila pakubwa katika siasa za uchaguzi mkuu ujao.

Wakati wa kuzinduliwa kwa Nakuru kuwa mji wa nne Kenya, Kenyata alitaka vijana kuunga mkono ‘Mzee’ ifikapo 2022, hiyo nin katika kile kilichoonekana kama kumlenga naibu wake William Ruto, Rais aliwataka vijana kutosisimka kutokana na ahadi wanazopewa.

Alisema kuna baadhi ya wanasiasa ambao walianza siasa zao mapema na watachoka kabla ya kumaliza mkondo. “Siasa sio kama mpira ule unachezwa uwanjani. Si kama mbio zile za kutimuka, hii ni marathon. Wewe ulianza ukaenda mbio shauri yako. Mzee alianza mosmos sasa utaishiwa na pumzi akupite tu,” Rais alisema.

“Inataka pole pole tu, usikimbie enda polepole na utapata. Unaweza kukimbia ukapata na hata ukipata ikuletee shida baadaye,” aliongeza Kenyata katika uzindui huo wa mji wa Nakuru.

Ni wazi kuwa urafiki kati ya Rais Uhuru Kenyatta na kinara wa ODM Raila Odinga unazidi kushika mizizi kila uchao ambapo wawili hao wamekuwa marafiki wakuu tangu wafanye makubaliano ya kisiasa kupitia mkataba wa handisheki.

Wawili hao wamekuwa wakiishi kama ndugu wa mama mmoja tangu walipofanya makubaliano ya kisiasa kupitia mkataba wa handisheki.

Ben Pol kutumbuiza jukwaa la amani Misri
Mwanaume aibuka na bango la kutafuta mke