Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta ametangaza kuwa serikali yake iliyopo madarakani itafanya zoezi la ukaguzi wa aina ya maisha wanayoishi wafanyakazi wa umma.

Amesema kuwa wafanyakazi wote wa umma akiwemo yeye mwenyewe na Makamu wake, William Ruto watatakiwa kutoa maelezo ya mali wanazomiliki na wale watakaobainika kuiba fedha za umma watawajibishwa kwa mujibu wa sheria.

Rais Kenyatta ameyasema hayo wakati ambapo nchi hiyo ikishuhudia kampeni kubwa ya kupambana na vitendo vya rushwa ambapo hivi karibuni maofisa kadhaa wa serikali walikamatwa na kufunguliwa mashtaka ya ubadhirifu wa mali za umma na matumizi mabaya ya ofisi.

Hata hivyo, siku za hivi karibuni, maafisa wa serikali na watu wengine zaidi ya 40 wameshtakiwa kwa wizi wa mamilioni ya Dola zilizokuwa zimetengewa kwa ajili shirika la huduma kwa vijana NYS.

 

China jino kwa jino na Marekani, yalipiza kisasi
Video: Askari amsubiri Magufuli juu ya mti, Tajiri ajitwanga risasi hadi kufa