Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini jana amefanya utenguzi katika nafasi ya waziri wa fedha, iliyokuwa ikishikiliwa na Stephen Dau na kumteua Salvatore Garang Mabiordit kuziba nafasi hiyo.

Rais Kiir pia alimwondoa Marial Chanoung katika nafasi yake ya Mkuu wa Operesheni,Mafunzo na Intelijinsia wa Jeshi la Ukombozi la Watu la Sudan, Chanoung  mmoja kati ya maofisa sita waandamizi wa serikali na wapinzani, waliowekewa vikwazo na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kutokana na kukwamisha mchakato wa amani, na kuzuia usambazaji wa misaada.

Mabadiliko hayo yalitangazwa kupitia radio ya serikali jana jioni na hayakuweka wazi sababu za kutimuliwa kwa maofisa hao.

Serikali yatangaza kuzitambua dawa tano za tiba mbadala
Young Africans waifuata Township Rollers