Rais wa Zambia, Edgar Lungu amekiri kuidhinisha kiasi kikubwa cha fedha kwa ajili ya kuwanunua madiwani wa chama kikuu cha upinzani katika ngome zao, lakini fedha hizo zimechakachuliwa na maafisa wake.

Rais Lungu amesema kuwa katika fedha alizoidhinisha kila diwani wa chama kikuu cha upinzani cha United Party for National Development (UPND) aliyekubali kuhamia chama tawala cha Patriotic Front (PF) alitakiwa kulipwa K200,000 na wengine K500,000, kulingana na ugumu wa eneo husika.

Hata hivyo, ameshtushwa kusikia kuwa madiwani hao wamelipwa kiasi cha K20,000 na K5000 (Kwacha 1 ni sawa na Sh 235 ya Tanzania).

“Bajeti niliyoletewa na kuidhinishwa, kila diwani wa UPDNP aliyekubali kujiuzulu na kujiunga na PF katika maeneo ya Kaskazini apewe K200,000 pamoja na kazi. Na wale wa majimbo ya Kaskazini Magharibi, Magharibi na Kusini wapewe K500,000 kila mmoja pamoja na gari la kazi, kwa sababu tusingeweza kutetea viti kule,” Rais Lungu alimwambia Davies Mwila.

Aliwashukia maafisa waandamizi wa chama chake kwa kufanya ufisadi wa fedha zilizotengwa kwa lengo la kujiimarisha kisiasa.

Baadhi ya madiwani wa UPND wamekiri kuwa walipewa kiasi kidogo cha fedha tofauti na kile walichoahidiwa na kwamba hawajapewa kazi wazoahidiwa pia.

Video: Lowassa amshukia Mkapa, Maagizo 9 ya JPM kwa wafanyabiashara
Hawaolewi kwasababu wanawaza starehe tu- Mbasha

Comments

comments