Rais wa Zambia Edgar Lungu amewataka wananchi kuachana na masuala ya siasa na kujikita katika kukuza maendeleo ya uchumi wa nchi.

Lungu ameyasema hayo leo jijini Dar es salaam wakati alipotembelea Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), TICTS na kampuni ya  bandari kavu ikiwa ni ziara yake ya siku tatu hapa nchini.

“Muda wa siasa umekwisha, wanasiasa wanakuja na kuondoka lakini maendeleo ya nchi yatabaki, hivyo kikubwa tujikite katika kujenga na kukuza uchumi kwa ajili ya nchi” alisema Rais Lungu.

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Edwin Ngonyani alisema kuwa ushirikiano baina ya Tanzania na Zambia ulianza kabla ya Uhuru ambapo reli ya TAZARA ilitumika katika kuunganisha nchi hizi mbili ambazo mpaka sasa zinashirikiana katika masuala tofauti.

Majaliwa azitaka halmashauri kuanzisha mashamba miti
Ndege iliyobeba wachezaji soka wa Brazil yaanguka, watu 76 wafariki dunia