Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amempigia debe Zinedine Zidane kurejea nchini humo huku kukiwa na taarifa kocha huyo atajiunga na Mabingwa wa Soka wa Ligue 1 PSG.

Macron, ambaye alichukua jukumu la kumshawishi Mbappe kubaki kwenye klabu hiyo, aliliambia taarifa hizo kupitia Jarida la RMC Sport,

“Sijazungumza na Zinedine Zidane, lakini ninavutiwa naye sana, akiwa mchezaji na kocha. Tunataka sana  kumuona Ufaransa, kocha mwenye kipaji ambaye ameweza kushinda makombe makubwa ambayo tunatamani sana kwa klabu zetu.

“Ni jukumu langu kusema kwamba Ufaransa ni taifa kubwa la michezo na mpira, kuna watazamaji wengi wanaopenda mchezo huu. Ni muhimu kwetu walio bora zaidi wawe hapa,” amesema rais huyo.

PSG inahusishwa na mpango wa kumtimua Kocha wake wa sasa Mauricio Pochettino, kufuatia kushindwa kufikia lengo la kutwaa Ubigwa wa Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya msimu uliopita 2022/23.

Serikali ya Zanzibar yaipongeza Benki ya NBC
Habari kuu kwenye magazeti ya leo Juni 10, 2022