Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli ametoa agizo kutafutwa kwa daktari aliyekimbia kufanya kazi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tabora kwa madai ya maslahi madogo na hatua zaidi kuchukuliwa.

Rais Magufuli ametoa agizo hilo leo Januari 30, 2021 wakati akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa jengo la magonjwa ya dharura katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tabora, ambapo akiwa katika eneo hilo ameagiza Madaktari waliohama Hospitali hiyo ya Serikali na kuhamia Hospitali binafsi kwa kigezo cha maslahi wafuatiliwe.

“Mtafuteni huyo Daktari aliyekimbia Hospitali ya Serikali na hiyo Hospitali binafsi aliyokimbilia, ikiwezekana tunamfungia Daktari, tunaifungia na Hospitali aliyoenda, wakati wa kusomesha hawatuchangii, tukishawasomesha wanakwenda kuwaiba, sio sawa” amesema Rais Magufuli.

“Madaktari wanapata mkopo 100% wakiwa Chuoni, halafu tunawapa ajira Serikalini wanakimbia kisa maslahi, si ungekimbia wakati unasoma?, hela yetu umekula halafu unakimbia kwenda Hospitali binafsi kwa kisingizio cha maslahi, ni kukosa uzalendo”  ameongeza Rais Magufuli.

Marufuku uagizwaji wa nyuzi za kufungia tumbaku
Kamanda wa Tanzania Prisons astaafu soka