Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli ameenda mapumziko katika Kijiji cha Mlimani wilayani Chato, Mkoa wa Geita.

Kwa mujibu taarifa iliyotumwa na Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu Gerson Msigwa, Rais Magufuli amewasili Wilaya ya Chato kwa ndege ya ATCL leo Julai 01, 2019, huku akipata fursa ya kusalimia na baadhi ya wananchi wa Chato.

Akizungumza na wananchi wa Chato Rais Magufuli amewapongeza wananchi kwa kuitikia wito wa Serikali wa kuongeza juhudi katika kazi za uzalishaji mali, hali iliyoiwezesha wilaya hiyo kupiga hatua kubwa za kimaendeleo.

“Nawapongeza sana wananchi wa Chato, mnachapa kazi kwelikweli na maendeleo yanaonekana, Chato inabadilika, nilishasema asiyefanya kazi na asile kwa hiyo tuendelee kushikamana kufanya kazi na kujenga nchi yetu” amesema Rais Magufuli.

Rais Magufuli pia ametoa wito kwa Watanzania wote kuendelea kuchapa kazi kwa juhudi na maarifa, kushikamana na kutobaguana ili kwa pamoja waijenge Tanzania ambayo ina rasilimali nyingi.

 

Rapa 50 Cent amkana mwanae hadharani
Mfungwa ajiua mbele ya mkuu wa gereza