Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli ameendelea kuibana Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), akieleza kutoridhishwa na utendaji wake.

Rais Magufuli amesema kuwa Mamlaka hiyo imeshindwa kuendana na kasi ya nchi nyingine za Afrika, ikijikita katika kuweka utitiri wa kodi na kuwabana walipa kodi badala ya kutengeneza fursa ya kuongeza idadi ya walipa kodi.

“Tuna wastani wa walipa kodi milioni 2.27, uwiano wa kodi inayokusanywa na Pato la Taifa (GDP) ni asilimia 2.8 ambacho ni kiwango cha chini ukilinganisha na nchi nyingine za Afrika. Kwenye suala la ukusanyaji wa mapato hatufanyi vizuri,” alisema Rais Magufuli.

Alieleza kuwa hata baadhi ya nchi za Afrika ambazo zina idadi ndogo ya watu, bado zina idadi kubwa ya walipa kodi ukilinganisha na Tanzania. Alitoa mfano wa Msumbiji ambao idadi ya watu ni karibu nusu ya Watanzania lakini idadi ya walipa kodi ni mara mbili ya Tanzania.

“Ikiwa Msumbiji wapo milioni 27 ila wana walipa kodi milioni 5.3, inakuwaje sisi ambao tuko milioni 55 tukawa na walipa kodi 2.2 milioni?” Alihoji Rais Magufuli na kuongeza kuwa hali hiyo inatokana na kukosa ubunifu wa kupanua wigo wa walipa kodi.

Aliongeza kuwa TRA wameshindwa zaidi katika ukusanyaji kodi wa za majengo akieleza kuwa kiwango cha nyumba zilizosajiliwa hakiridhishi.

Mbali na ukusanyaji wa mapato, takwimu zinaonesha kuwa hadi mwaka jana biashara 200,000 zilifungwa kwa sababu mbalimbali hali inayoziba mianya ya mapato ya Serikali pia.

Hivi karibuni, Rais Magufuli alitoa vitambulisho jumla ya vitambulisho 670,000 kwa ajili ya wafanyabishara wadogo ili kurasimisha biashara zao ambapo kila mkoa umepewa vitambulisho 25,000. Mfanyabiashara mdogo atalipia shilingi 20,000 kupata kitambulisho hicho.

Museveni azindua kitengo cha kupambana na rushwa
Video: JPM apiga 8 nzito, Dkt. Bashiru uso kwa uso na Membe, Hujuma kubwa, Msajli ajibu hoja vyama vya siasa