Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli amefanya mabadiliko kwa Wakuu wa Wilaya kwa kumteuwa Deogratius Ndejembi kuwa mkuu mpya wa Wilaya ya Kongwe Mkoani Dodoma na kumhamisha John Ernest Palingo kwenda wilaya ya Mbozi.

Mabadiliko hayo yamefanywa na Rais Magufuli baada ya kuridhia maombi ya Bw. Ally Masoud Maswanya aliyeteuliwa kuwa mkuu wa Wilaya ya Mbozi, kuomba kutenguliwa kwa sababu ninafsi.

Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi amesema, Bw. Deogratius Ndejembi atakula kiapo cha uadilifu kwa Viongozi wa Umma siku ya Jumanne tarehe 12 Julai 2016 Ikulu, Jijini Dar es salaam.

Rais Magufuli Ateuwa Wakurugenzi
Video: Taifa letu kwa sasa linahitaji Uongozi wenye kuona mbali - Majaliwa