Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli leo August 13, 2018 amefanya uteuzi na mabadiliko madogo ya Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi katika halmashauri mbalimbali.

Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi amesema wakurugenzi wote walioteuliwa kwa mara ya kwanza wanatakiwa kuripoti siku ya jumatano Agosti 15, 2018 katika ofisi ya Tamisemi na wale ambao wamefanyiwa mabadiliko ya vituo vyao vya kazi kuripoti katika vituo vyao vya kazi mara moja kuanza kazi.

Uteuzi huo ni kama ifuatavyo;

Amemteua Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Msafiri Simeoni na kumpelekwa Chato, na Senyi Simon amepelekwa Kwimba.

Pia amefanya uteuzi wa Wakurugenzi wa Halmashauri na Majiji kama ifuatavyo.

Halmashauri ya Misenyi Mkurugenzi ni Innocent Mbandwa

Jiji la Mbeya Mkurugenzi ni James Kasusura

Halmashauri ya Malinyi Mkurugenzi ni Mussa Elias Mnyeti

Mkurugenzi wa Jiji la Arusha ni Maulid Madeni

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Temeke ni Lusibilo Mwakabili

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ubungo ni Beatrice Kwai

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kigamboni ni Mwilabu Nyabusu

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kondoa mkoani Dodoma ni Mustapha Yusuph

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Moshi ni Tatu Seleman Kikwete

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kakonko ni Masumbuko Stephano

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Katavi ni Ramadhan Mohamed

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Butiama ni Mugalane Alphonce

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kyela ni Lucy Mganga

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kilombelo ni Eng. Stephan Kaliwa

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kilosa ni Asailiwe Lucas

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ukerewe ni Esther Chaula

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Meru ni Emmanuel Mkongo

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Simiyu ni Michael John

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ikungi ni Justice Laurenc

Install Application ya Udaku Special Uweze Pata Habari Kirahisi Zaidi

Mbunge wa CUF ajiunga CCM
AY na mkewe wapata mtoto wa kiume, ataja jina na maana yake