Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanazania John Pombe Magufuli amefanya uteuzi mwingine na kumteua Balozi Dkt.  Aziz Ponary Mlima kuwa Balozi wa Tanzania nchini Uganda.

Kufuatia uteuzi huo Balozi Mlima anatarajia kuapishwa leo Septemba 12, 2018 Ikulu Chamwino, Jijini Dodoma.

Pia Septemba 3, 2018 Rais Magufuli alifanya uteuzi wa Dkt. John Antony Kiang’u Jingu kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ambapo kabla ya uteuzi huo Kingu alikuwa Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambaye naye atakula kiapo leo.

Aidha, naye Kamishna wa Polisi Diwani Athumani aliyeteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU anatarajia kuapishwa leo Chamwino Jijini Dodoma.

Makala: Nyota ya Mwakinyo inavyofanana na ya Pacquiao (video)
Kocha wa Brazil amjibu Trump