Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli leo tarehe 25 April 2016 amefanya uteuzi wa Makatibu Tawala wa Mikoa 26 ya Tanzania Bara. Taarifa imetolewa leo na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, ameeleza kuwa kati ya Makatibu tawala hao 10 ni wapya, 2 wamebadilishiwa vituo vya kazi na 13 wamebakia katika vituo vyao vya sasa.

Makatibu Tawala wapya walioteuliwa hawa hapa;
⦁> Arusha – Richard Kwitega
⦁ >Geita – Selestine Muhochi Gesimba
⦁> Kagera – Armatus C. Msole
⦁> Kilimanjaro – Eng. Aisha Amour
⦁> Pwani – Zuberi Mhina Samataba
⦁> Shinyanga – Albert Gabriel Msovela
⦁> Singida – Dr. Angelina Mageni Lutambi
⦁> Simiyu – Jumanne Abdallah Sagini
⦁ >Tabora – Dkt. Thea Medard Ntara
⦁> Tanga – Eng. Zena Said

Makatibu Tawala waliobadilishwa vituo vya kazi hawa hapa;
⦁> Kigoma – Charles Amos Pallangyo (Kutoka Mkoa wa Geita)
⦁> Morogoro – Dkt. John S. Ndunguru (Kutoka Mkoa wa Kigoma)

Makatibu Tawala waliobakishwa katika vituo vyao vya sasa vya kazi ni kama ifuatavyo;
⦁> Dar es salaam – Theresia Louis Mbando
⦁> Dodoma – Rehema Hussein Madenge
⦁> Iringa – Wamoja Ayubu Dickolagwa
⦁> Katavi – CP Paul Chagonja
⦁> Lindi – Ramadhan Habibu Kaswa
⦁> Mara – Benedict Richard Ole Kuyan
⦁> Manyara – Eliakimu Chacha Maswi
⦁> Mbeya- Mariam Amri Mjunguja
⦁> Mtwara – Alfred Cosmas Luanda
⦁> Mwanza – CP. Clodwing Mathew Mtweve
⦁> Njombe – Jackson Lesika Saitabau
⦁> Rukwa – Symthies Emmanuel Pangisa
⦁> Ruvuma – Hassan Mpali Bendeyeko
Makatibu Tawala wa Mikoa wapya ambao wameteuliwa kwa mara ya kwanza, wataapishwa siku ya Jumatano tarehe 27 Aprili, 2016 saa tatu asubuhi Ikulu Jijini Dar es salaam.

TFF Yaingilia Kati Sakata La Uchaguzi Wa Young Africans
Odion Ighalo Apata Pigo Mara Mbili Ndani Ya Saa 24