Leo Julai 23, 2018 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli amekabidhiwa Hundi za fedha zenye Thamani ya zaidi ya Shilingi  Bilioni 700 kama gawio la Serikali kutoka Taasisi na Mashirika ya Umma na kampuni zilizobinafsishwa.

Tunatoa pongezi kwa kazi nzuri anayoifanya Rais Magufuli kusimamia kwa uweledi na kuonesha maarifa makubwa katika suala hilo kwani miaka ya nyuma lilisahaulika na kupuuzwa.

Huko nyuma masharika machache yalikuwa yakitoa gawio kwa serikali tena kwa kiwango cha chini kulinganisha na sasa ambapo mashirika yamejitokeza kwa wingi na hata yale ambayo yalikuwa hayatoi awamu hii yamejitokeza na kutoa gawio kwa serikali.

Aidha kiasi hiko cha pesa, Bilioni 723 zitasaidia kuongeza huduma mbalimbali ikiwemo ujenzi wa vituo vya afya katika maeneo mbalimbali ya vijijini, pia itasaidia kugharamia ujenzi wa miradi mikubwa ya maendeleo kama vile barabara za vijijini na mijini pamoja na changamoto nyingine kama ulipaji wa mishahara  kwa watumishi wa umma wakiwemo walimu wa shule za kata.

 

 

 

Video: Clement Sanga afunguka kilichomuondoa Yanga
Kovacic aomba kuondoka Real Madrid

Comments

comments