Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh.Dkt John Joseph Pombe Magufuli kupitia kwa katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano,Dkt Leonard m.Chamuriho,Amemteua prof.Ignas Aloys Rubaratuka kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya mamlaka ya Bandari Tanzania TPA.katika kipindi cha miaka (3)kuanzia tarehe 21/04/2016

Hayo yamesemwa na Katibu mkuu wa wizara hiyo Dkt.Leonard Chamuhiro alipokua akiongea na waandishi wa habari mapema hii leo jijijni Dar es salaam,Chamuhilo alisema kwa mujibu wa sheria na.17 ya mwaka 2004 ya mamlaka ya usimamizi wa bandari(TPA)kifungu cha 6(2)(A)rais anamamlaka ya kufanya uteuzi mwenyekiti wa bodi.Prof.Ignas Aloys ni mhadhiri mwandamizi wa chuo kikuu cha Dar es salaam.

Aidha Waziri Mwenyedhamana ya sekta ya uchukuzi Mh,Prof.Makame Mbarawa(MB), kwa mamlaka aliyopewa kwa mujibu wa kifungu na.6(2)(b)cha sheria na.17 ya mamlaka ya usimamizi wa bandari Tanzania(TPA)ya mwaka 2004 amewateua wafuatao kuwa wajumbe wa Bodi ya wakurugenzi wa mamlaka ya usimamizi wa bandari Tanzania kuanzia Tarehe 14/06/2016,kwa muda miaka(3).

Walioteuliwa pamoja na Bw,Jaffeer Salim Mchano, Mkurugenzi wa mipango na huduma, Tanzania Investiment Bank,Eng,Deusdedit Conatus Vitalis Kakoko, Meneja miradi,Tanrod,Bw,Malata Gabriel Pascal, Mkurugenzi msaidizi,Division of litigation and arbitration, na Dkt,Jabir Kuwe Bakari kuwa mkurugenzi mkuu wakala wa serikali mtandao,Ofisi ya rais,utmishi na utawala bora, 

Wenguine walioteuliwa ni kama ifuatavyo,

Bw,Masanja kungu Kadogosa kaimu mkurugenzi mkuu kampuni ya reli Tanzania (TRL),

Bw Aziz Massala kilonge kuwa mkurugenzi mtendaji na mshauri mwelekezi Amak Consulting,

Dkt Francis k.Michael kuwa mhadhiri mwandamizi katika chuo kikuu cha Dar es salaam(DSM) na

Jayne Kezier Nyimbo kuwa mtaalamu wa rasilimali watu na meneja mtendaji Carteck, Tanzania

Vile vile katibu mkuu huyo kupitia uteuzi wa viongozi hao wametakiwa kuripoti katika vituo vyao mara tu wapatapo taarifa kuhusu uteuzi wao.

Video: Seneta na Gavana wazichapa kwenye kikao Kenya
Neema yatarijiwa Vyuo vikuu.