Mtoto wa aliyekuwa gwiji wa masumbwi duniani (Mohammed Ali) Laila Ali amekoshwa na kitendo cha Rais Magufuli kutilia mashaka vifaa vinavyoingizwa nchini kwa ajili ya kukabiliana na mlipuko wa virusi vya Corona

Kupitia bandiko aliloliweka katika ukurasa wake wa Instagram LailaAli amesema watu wanapaswa kufanya utafiti binafsi kwa manufaa ya familia zao muda wote.

Laila (43) ni mtoto wa nane kati ya tisa kwenye familia ya marehemu Mohammed Ali, kwa sasa ni mtangazaji wa televisheni lakini awali aliwahi kuwa bondia ambapo alicheza masubwi kati ya mwaka 1999 na 2007 na kufanikiwa kutwaa ubingwa wa WBC, WIBA, IWBF pamoja na IBA uzito wa kati (Wanawake).

TANZIA: Mkuu wa wilaya ya Nyang'wale afariki dunia
Ander Herrera: Sikutaka kuondoka Man UTD