Rais John Magufuli leo amempa Mrisho Mpoto sababu nyingine ya kuendelea kuongeza nguvu kwenye muziki wake baada ya kumhakikishia kuwa wimbo wake wa ‘Sizonje’ ni ‘hit song’ inayokubalika Ikulu.

Mpoto ambaye alikuwa miongoni mwa ‘wananchi’ waliofika katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kumpokea Rais Magufuli akitokea mikoa ya Kanda ya Ziwa, alipata furaha kuu baada ya Mkuu huyo wa nchi kumueleza kuwa anaujua wimbo wa ‘Sizonje’ na kwamba ni miongoni mwa nyimbo anazozipenda sana.

Rais John Magufuli akifurahia jambo na Mrisho Mpoto

Rais John Magufuli akifurahia jambo na Mrisho Mpoto

“Naujua #SIZONJE moja ya nyimbo zangu bora kabisa,” Maneno ya Mh. Rais leo,” Mrisho Mpoto ameandika kwenye Instagram.

Mapema Mwaka huu, Mpoto aliachia wimbo na video ya wimbo huo aliomshirikisha Banana Zorro, na uligeuka kuwa wimbo mkubwa.

Wacomoro Kuchezesha Serengeti Boys, Afrika Kusini
Video Mpya: Dully Sykes Feat. Harmonize