Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amemtaka Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Charles Kichere kutelekeza maagizo atakayopewa na mihimili mingine na kufanya kazi bila kuonea watu.

Rais Magufuli amesema hayo leo Novemba 4, 2019 wakati akimuapisha Kichere kuwa CAG mpya pamoja na wateule wake wengine Ikulu jijini Dar es Salaam.

Unapopewa kazi na mihimili mingine kama Bunge au Mahakama kaitekeleze usibishane nao wewe ni mtumishi.” Amesema Rais Magufuli

Rais Magufuli amemtaka kufanya kazi bila kuonea watu na asijifanye kuwa ni mhimili kwani kuna mihimili mitatu pekee.

“Nafasi yako ni mkaguzi mkuu wa Serikali, kwa hiyo mwenye Serikali yupo, kafanye kazi zako vizuri bila kuonea watu,” amesema Rais Magufuli.

Wadanganyifu mitihani kidato cha nne waonywa

Aidha, Rais Magufuli amemwagiza CAG Kichere kwenda kusimamia ofisi kwani kuna baadhi ya watendaji wanaomba fedha wanapokwenda kukagua balozi.

Amesema, “ Kasimamie hiyo ofisi kuna baadhi ya watendaji wako wanapokwenda kukagua kwenye balozi wanaomba fedha, sasa nenda kawachambue.”

“Ofisi ya CAG sio clean (safi) kama mnavyofikiria, sasa nenda kachambue ukapange ‘positions’ (nafasi) za watu wako, ili mauchafu (uchafu) haya ukayasafishe.

Charles Kichere ameteuliwa na Rais Magufuli jana Novemba 3, 2019 kuwa CAG wa 7 ambapo tayari ameapishwa leo Novemba 4, 2019 na anatarajiwa kuanza kazi kesho.

Jafo: Muda wa kuchukua fomu hautaongezwa " Msifunge ofisi"
Ndugai afunguka CAG Kichere anavyotegemewa