Rais John Magufuli, leo amemteua Jaji Ferdinand Leons Wambali kuwa Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania.

Kwamujibu wa taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Ikulu, uteuzi huo wa Jaji Wambali unaanza mara moja tangu ulipotangazwa.

Jaji Wambali ambaye kabla ya uteuzi huo alikuwa Mkuu wa Chuo Cha Uongozi wa Mahakama Lushoto kilichoko mkoani Tanga, anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Jaji Shaabani Ally Lila ambaye aliteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani.

 

 

wananchi watakiwa kuchukua tahadhari juu ya mabadiliko ya hali ya hewa yanayojitokeza
NEC yamkabidhi Magufuli bilioni 12 zilizobaki katika uchaguzi mkuu