Rais John Magufuli leo amemteua mwenyekiti wa chama cha Tanzania Labor Party (TLP), Augustine Mrema kuwa mwenyekiti wa Bodi ya Parole.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na Kurugunzi ya Mawasiliano ya Ikulu, Mrema ameteuliwa kushika nafasi hiyo kwa kipindi cha miaka 3 akichukua nafasi iliyoachwa wazi na Jaji Mstaafu, Eusebia Nicholaus Munuo aliyemaliza muda wake.

Uteuzi huu unaweza kutafsiriwa kama kutimizwa kwa ahadi aliyoitoa Rais Magufuli wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu alipokuwa katika jimbo la Vunjo. Rais Magufuli aliahidi kumpa kazi Mrema ambaye alijitokeza kumlaki na kumnadi ingawa chama chake kilikuwa na mgombea urais pia.

Augustine Mrema

Mbali na Mrema, wengine walioteuliwa leo na Rais Magufuli ni pamoja na Prof. William Mahalu ambaye anakuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete na Prof. Mohamed Janabi kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo.

Young Africans Yajichimbia Kaburi Kombe La Shirikisho
AY alivyopewa zawadi ya saa ya zaidi ya shilingi milioni 16 na Jose Chameleon