Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli amewapandisha vyeo maafisa wanne wa Jeshi la Magereza kutoka Naibu Kamishna wa Magereza (Deputy Commissioner of Prisons – DCP) hadi kuwa Kamishna wa Magereza (Commissioner of Prisons – CP).

Maofisa hao ni Hamis Ngarama, Tusekile Mwaisabila, Augustine Sangalali Mboje, Gideon Marco Nkana.

Pia amewapandisha vyeo maafisa wa Jeshi la Magereza wengine 5 kutoka Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza (Senior Assistant Commissioner of Prisons – SACP) hadi kuwa Naibu Kamishna wa Magereza (Deputy Commissioner of Prisons – DCP).

Ambao ni Julius Mayenga Sang’udi, Afwilile Mwakijungu, John William Masunga, Phaustine Marint Kasike, Joram Yoram Katungi.

Uteuzi huo umefanyika mapema leo hii Juni 2, 2018.

 

Hamisa aibariki ndoa ya Diamond na Zari
Ferguson aruhusiwa kutoka Hospitali