Leo Mei 28, 2018 jijini Dar es salaam, Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amefanya kikao na Kamati Kuu ya Halmashauri ya Taifa ya CCM na NEC ambapo amesema ameridhia kujiuzulu kwa aliyekuwa Katibu Mkuu wa chama hicho, Abdulrahman Omar Kinana ambaye ametumikia nafasi hiyo kwa muda mrefu.

Rais Magufuli amesema kuwa yeye na Rais wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein wamekubali ombi la Kinana ili aweze kupumzika kwani amefanya kazi kubwa katika nafasi yake sasa anahitaji kupumzika.

“Nikatambua pia umri wa muheshimiwa Kinana nikamwita mzee Shein, akaniambia kwakweli tumkubalie” amesema Rais Magufuli.

Aidha, Rais Magufuli amesema anatambua mchango mkubwa wa katibu Mkuu huyo na kuongezea kuwa amekuwa akiomba kujiuzulu nafasi hiyo zaidi ya mara mbili na amekuwa akiomba kisirisiri hivyo wameamua kumkubalia.

 

 

 

Magazeti ya Tanzania leo Mei 29, 2018
Maafisa wa Marekani watua Korea Kaskazini, wateta ya Trump-Kim