Rais John Magufuli leo ametembelea na kusali katika kanisa la Maombezi linaloongozwa na Mchungaji Antony Lusekelo maarufu kama ‘Mzee wa Upako’ lililoko Ubungo jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika ibada hiyo, Rais Magufuli ameeleza kuwa huwa anafuatilia na kuyapenda mahubiri yanayotolewa na Mchungaji huyo ikiwa ni pamoja na huduma ya maombezi inayorushwa pia kupitia vipindi vya runinga.

“Mimi ni mfuatiliaji mzuri sana wa mahubiri yako, kwahiyo mahubiri unayoyatoa yanasambaa kwakweli mimi na familia yangu huwa yanatubariki sana. Kwahiyo nataka kukuhakikishia ninakupenda sana,” alisema Rais Magufuli.

Katika hatua nyingine, Rais Magufuli aliahidi kutengeneza barabara inayopita katika kanisa hilo kutoka Ubungo Kibangu hadi River Side na kuungana na barabara ya Mandela.

Mzee wa Upako2

Rais Magufuli alisema kuwa alisikia kilio cha Mzee wa Upako pamoja na wananchi wa eneo hilo kuhusu ubovu wa barabara na alimtuma Meneja wa barabara wa mkoa wa Dar es Salaam ambaye alifanya upembuzi yakinifu na kuandaa mpango wa kuitengeneza.

“Nataka nikuthibitishie kuwa fedha za kutengenezea barabara hii zipo,” alisema Rais Magufuli.

Mzee wa Upako alimshukuru Rais Magufuli kwa kulitembelea kanisa hilo na kumuombea heri katika utawala wake.

CUF watangaza kuziba nafasi ya Lipumba na Duni
Waliotimuliwa UDOM wang’aka, “Sisi sio Vilaza”