Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Sivangilwa Sikalalilwa Mwangesi (Jaji wa Mahakama ya Rufani) kuwa Kamishna wa Maadili.

Mwangesi ameteuliwa kushika wadhifa huo baada ya Jaji wa Mahakama ya Rufani Mstaafu Harold Nsekela kufariki dunia.

Uteuzi wa Mwangesi unaanza leo tarehe 23 Desemba, 2020 na ataapishwa kesho tarehe 24 Desemba, 2020 saa 4:00 asubuhi, Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma.

Wakulima waaswa kutumia mbegu bora
Mpango awapa siku 9 waliochangia chini ya kiwango