Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amefanya mabadiliko madogo ya uongozi na kumteua Bw. Mrisho Gambo kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha kuanzia mapema leo (Alhamisi, Agosti 18,2016).

Akizungumzia uteuzi huo Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema Bw. Gambo anachukua nafasi ya aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo, Bw. Felix Kijiko Ntibenda ambaye uteuzi wake umetenguliwa.

Amesema Bw. Ntibenda anahamishiwa Ofisi ya Waziri Mkuu ambako atapangiwa majukumu mengine.

Kabla ya uteuzi huo, Bw. Gambo alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Arusha. Ataapishwa kesho (Ijumaa, Agosti 19, 2016) saa 3 asubuhi Ikulu jijini Dar es Salaam.

Mario Gomez Arejea Nyumbani, Vurugu Za Kisiasa Zamkimbiza Uturuki
Riyad Mahrez Afunga Mjadala, Ajitia Kitanzi Hadi 2020