Rais John Magufuli amefanya uteuzi wa Wakurugenzi wakuu wapya wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC), Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) na Kampuni Hodhi ya Rasilimali za Reli Nchini (RAHCO).

Taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Ikulu imemtaja Profesa Godius Kahyarara kama mteule wa Rais kuwa Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, akichukua nafasi iliyoachwa wazi na Dk. Ramadhani Dau.

Dk. Dau aliteuliwa awali na Rais kuwa Balozi japo bado hajapangiwa nchi atakayoenda kufanya kazi hiyo ya kidiplomasia.

Kadhalika, Rais Magufuli amemteua Ayub Rioba Chacha kuwa Mkurugenzi Mkuu wa TBC akichukua nafasi ya Clement Mshana ambaye amestaafu.

Dk. Issa Iddi Mgwatu pia ameteuliwa na Rais Magufuli kuwa Mkurugenzi Mkuu wa RAHCO akichukua nafasi iliyoachwa wazi na Mhandisi Benhadard Tito, ambaye uteuzi wake umetenguliwa na Rais.

Uteuzi

Hii hapa kauli ya mwisho ya Jecha kabla ya kuanza upigaji kura Zanzibar
Makonda adai hata akifa ameshafanikiwa, atangaza vita kali na wauza Unga