Kufuatia mauaji ya watoto saba mkoani Njombe Rais John Pombe Magufuli ametoa salamu za pole kwa wafiwa na kuwachangia shilingi milioni tano kama sehemu ya rambirambi yake.

Akihutubia mkoani humo amesema kuwa suala la mauaji ya watoto mkoani humo limetia doa kubwa kutokana na imani za ushirikina.

Amewaomba viongozi wa dini kutoa mafundisho kuhusu matendo ya kweli na kuhakikisha watu wanaachana na imani za ushirikina kwani hazina tija katika maendeleo yao kama ambavyo inaaminika na baadhi ya watu.

”Huwezi kutajirika kwa kuua watoto, sa nyingine unaua watoto wako, mimi sijatia sahihi kunyonga lakini nikiletewa kesi kama hii nitamuomba malaika wangu inawezekana nikasaini, haiwezekani tukaendekeza mambo ya ushirikina” amesema Rais Magufuli.

Ameomba kitendo kama hicho kisijirudie tena kwani kinaleta doa kubwa kwa mkoa huo.

Aidha amesifia uchapaji kazi wa watu wa mkoa wa Njombe.

Magufuli atengua na kusamehe Njombe
Rais Magufuli ataja sababu ya kumtumbua RPC Njombe

Comments

comments