Juni 26 mwaka huu Rais John Pombe Magufuli alitangaza kuteua Wakuu wa Wilaya zote nchini, na Wakuu wa Mkoa watatu. Kati ya Wakuu wa Wilaya 139 walioteuliwa, 39 wamebakishwa katika nafasi zao huku 100 wakiwa ni wapya.

Katika hali ya kushangaza siku moja baada ya orodha hiyo kutangazwa, Rais Magufuli ametengua uteuzi wa mkuu wa wilaya ya Ikungi iliyopo mkoani Singida. Rais Magufuli alitengua uteuzi wa Bwana Fikiri Avias Said ndani ya masaa 24 tangu uteuzi wake.

Sababu kuu ya Rais kutengua Uteuzi huu ameisema leo hii wakati wa hafla ya kuwaapisha Wakuu wote wa wa wilaya walioteuliwa, ni kwamba jina lilikosewa, na kusema kwamba Mkuu wa Wilaya halali wa Ikungi ni Bwana Miraji Mtaturu ambaye ni Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Mwanza,

Zilikuwepo fununu  kwamba Fikiri Avias Said mara baada ya kuona jina lake kwenye orodha ya Wakuu wa Wilaya iliyotoka wikiendi hii aliwasiliana na viongozi wa Ikulu na kukataa nafasi hiyo. Hivyo basi yeye mwenyewe ndio aliomba kuondolewa kwenye nafasi hiyo. Fununu hizi hazina ukweli wowote

Ombi la kukifuta Chama Cha Wananchi (CUF) latua Bungeni
Video: Serikali kuwatengea maeneo zaidi wachimbaji wagodo wa Madini nchi nzima