Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ametoa siku 30, kwa baadhi ya makampuni ambayo yamekuwa yakijihusisha na ukwepaji kodi, kwa kuanzisha Makampuni hewa ya nje na baadaye kuomba punguzo la bei ya thamani kwa bidhaa wanazoziuza nje ya nchi.

Ameyasema hayo Ikulu jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza na Wafanyabiashara kutoka Wilaya 139 nchi nzima, ambao amewaita kwaajili ya kujadili changamoto za biashara nchini.

“Nimefuatilia baadhi ya wafanyabiashara wanatumia mbinu mbalimbali kukwepa kodi, kwa kudai marejesho ya kodi ya ongezeko la thamani (VAT), wakati mauzo yaliyofanyika ni mauzo hewa kutoka kwa Makampuni ya nje, nina orodha ya Makampuni 17,446, ambayo yamehusika na tuhuma hizi,”amesema Rais Magufuli

Aidha, amehoji kuwa labda ni kiongozi wao lakini mkutano ukimalizika atawapa orodha ya Makampuni hayo ili wakayafanyie uchambuzi na yale makampuni yatakayobainika yakajipange kulipa ndani ya siku 30.

Rais Magufuli amekutana na wafanya biashara watano kutoka kila wilaya nchini ambao wamewawakilisha wenzao, lengo ikiwa ni kufahamu matatizo yanayowapata.

 

Nyota 7 wa Taifa Stars kukosa mashindano ya AFCON
Aliyefungwa jela miaka 18 aachiwa akiwa na umri wa miaka 100