Novemba 6, 2016 katika kijiji cha Salala kilichopo Wilayani Shinyanga katika Mkoa wa Shinyanga watu 18 wamepoteza uhai na wengine 3 kujeruhiwa baada ya gari dogo aina ya Noah lililokuwa limebeba abiria 21 kugongana uso kwa uso na Lori majira ya saa moja jioni.

Kufuatia vifo hivyo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli ametuma salamu za rambirambi kwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainabu Taleck, ambapo ameeleza kusikitishwa na ajali za barabarani zinazoendelea kutokea huku akivitaka vyombo vinavyohusika na wadau wa usalama barabarani kushiriki kukabiriana na ajali hizo.

Amesema jambo hilo linaumiza sana kupoteza idadi kubwa ya watu namna hiyo, hivyo amemtaka mkuu wa Mkoa huo kufikisha salamu zake kwa familia za Marehemu wote, ndugu, jamaa na marafiki waliopoteza jamaa zao.

Rais Magufuli pia amemtumia salamu za rambirambi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein kufuatia kifo cha Mwenyekiti Mstaafu wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar, Jaji Zubeir Juma Mzee kilichotokea jana Novemba 7, 2016 mjini Unguja, na kifo cha Naibu Katibu Mkuu Mstaafu wa CCM, Saleh Ramadhan Ferouz kilichotokea usiku wa kuamkia leo Novemba 8, 2016 Unguja.

Magufuli ameeleza kupokea kwa masikitiko makubwa taarifa zote za msiba wa viongozi wastaafu, amesema “Tutawakumbuka kwa mchango wao mkubwa kwa Zanzibar na Taifa kwa ujumla kwa kuwa kipindi chote cha uongozi wao walijitahidi kutimiza wajibu wao na kuleta manufaa kwa Taifa”

Video: Mtoto wa marehemu Samuel Sitta asimulia kifo cha baba yake

Diego Milito Ampigia Debe Leonardo
Sababu za kukoroma ukiwa umelala na jinsi ya kuzuia hali hiyo.