Juhudi za kupambana na rushwa, ufisadi na umasikini zinazofanywa kiongozi wa awamu ya tano Rais wa jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Magufuli zimewafanya kila siku wasomi na wanaharakati kuamka na kupongeza kila hatua.

Mjumbe wa halmashauri kuu wa CCM Dkt Harun Kondo amesema jitihada za Rais Magufuli zinapaswa kuungwa mkono kwani anarekebisha udhaifu wote ambao ulijitokeza hapo nyuma na kiongozi huyuameonekana kuchukizwa nao.

Dkt Kondo amesema kuwa mwenendo wa rais Maufuli umewachukiza mafisadi wengi ambao hawalitakii mema taifa hili huku miongoni mwao wakiendelea kubeza juhudi hizi na kuwataja kuwa ni wanasiasa uchwara.

‘roho mbaya imechangia taifa letu kudumaa kimaendeleo kutokana na ubinafsi wa baadhi ya viongozi wetu wakiwemo wanasiasa, wafanyabiashara, watumishi wa umma wasomi hata wananchi wa kawaida”- Kondo.

Hata hivyo amesisitiza kuwa suala la ubinafsi nchini linatakiwa kupingwa kwa nguvu zote kwani ndilo linalosababisha kudorora huku watanzania kutopenda vitu vya nyumbani hali iliyopelekea kufa kwa viwanda vingi vya Tanzania.

Tumeua kiwanda cha general tyre lakini tunanunua YANA toka Kenya,  tumeua viwanda vingi kama kile cha betri za gari YUASA , Mashine too, Mang’ula na vingine vingi kwa sababu ya ubinafsi alisema Kondo.

Ugaidi: Watu 80 wauawa kwa risasi wakisherehekea Ufaransa
Video: Waziri Possi Ataka Watu Wenye Ulemavu kupewa kipaumbele