Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli amewashukuru viongozi wote wa dini nchini kwa kuendelea kuliombea Taifa na kudumisha amani na utulivu.

Dk. Magufuli ametoa shukrani hizo mapema leo Septemba 25, 2016 pamoja na mkewe, mama Janeth Magufuli walipo ungana na Waumini wa kanisa la Aglikana la Mtakatifu Albeno lililopo Posta jijini Dar es salaam kusali ibada ya jumapili.

Dk. Magufuli amesisitiza kuwa viongozi wa dini wanafanya kazi kubwa na mubimu katika Taifa, hivyo Watanzania wote bila kujali dini zao, itikadi zao za kisiasa, makundi na kanda zao wana wajibu kuungana na viongozi hao ili nia hiyo njema iendelee kufanikiwa.

 

Jina La Bob Bradley Laibuka Liberty Stadium
Majaliwa aagiza doria kuimarishwa kupambana na uvuvi haramu