Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amemaliza ziara yake ya kikazi ya siku 6 Mkoani Arusha leo Septemba 25, 2017 ambapo tayari amewasili Jijini Dar es salaam mara baada ya kumaliza ziara yake.

3

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda pamoja na viongozi wengine wa Mkoa wa Dar es Salaam mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere(JNIA) jijini Dar es Salaam wakati akitokea Mkoani Arusha.

2

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam wakati akitokea Mkoani Arusha.

4

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda pamoja na viongozi wengine mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam wakati akitokea Mkoani Arusha.

Video: Tushikamane kuleta maendeleo bila kubaguana - JPM
Rais Magufuli amaliza ziara mkoani Arusha