Siku chache baada ya kiwanda cha saruji cha bilionea wa Nigeria, Aliko Dangote kilichoko Mtwara kutangaza kusitisha shughuli zake kutokana na mzigo wa gharama za uzalishaji, bilionea huyo ameazimia kumuona Rais John Magufuli, ikulu jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa muwakilishi wa Dangote nchini, Esther Baruti, tajiri huyo amepanga kuja nchini ili azungumze na Rais Magufuli kuhusu kilichokisibu kiwanda chake hicho chenye mtaji wa zaidi ya dola za kimarekani milioni 500.

Hata hivyo, Baruti alifafanua kuwa kampuni yao haina tatizo lolote na Serikali kwani wamekuwa wakipewa msamaha wa kodi kwenye mambo mengi yanayohuisha uzalishaji.

“Kuna mambo mengi tuliyokubaliana na Serikali kabla ya kuwekeza kwenye mradi huu mkubwa na hatuna tatizo na serikali. Imetupa msamaha wa kodi kwenye mambo mengi kuanzia ardhi, mafuta ya dizeli lita milioni tatu na mengine mengi,” Baruti anakaririwa na Nipashe.

Wiki mbili zilizopita, Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda hicho kikubwa zaidi Afrika Mashariki, Harpreet Duggal alitangaza kusitisha kwa uzalishaji akieleza kuwa wamefikia uamuzi huo kutokana na kuongezeka kwa gharama za uzalishaji.

Mzee wa Upako amvaa askari polisi aliyemkejeli kuhusu ‘sadaka na ulabu’
Video Mpya: Vanessa Mdee: Cash Madame