Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, DKT John Pombe Magufuli, Rais mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete wameshiriki pamoja na waumini wengine kuaga mwili wa msanii mkongwe wa filamu nchini Amri Athuman maarufu kama Mzee Majuto katika viwanja vya Karimjee.

Viongozi wengine waliohudhuria shughuli hizo za kuaga ni Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Pwani, Zainab Vullu, Mufti wa Tanzania, Abubakar Zubeir, Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Musa Salum na  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.

Kadhalika mamia ya wasanii wamefika katika viwanja hivyo kwa ajili ya kutoa heshima za mwisho kwa msanii huyo mchekeshaji mahiri nchini akiwemo msanii Diamond Platinumz.

Majuto alifariki dunia jana majira ya saa mbili usiku katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili alipokuwa akipatiwa matibabu.

Aidha mwili wa mzee Majuto umesafirishwa kwenda nyumani kwake jijini Tanga ambako atazikwa kesho Ijumaa 10, Agosti 2018 mchana.

 

Gari la Mbunge wa Chadema lapata ajali mbaya
Waliopiga Sh28.5 bilioni za Nida wachemshiwa dawa