Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John pombe Magufuli anatarajia kufanya ziara ya siku mbili mkoani Njombe baada ya kutokea mkoani Ruvuma na kukagua baadhi ya miradi mikubwa ikiwemo ya barabara na hospitali

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Christopher Ole Sendeka alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, ambapo amesema kuwa Rais Magufuli atafanya ziara ya siku mbili kuanzia tarehe 09-10/04/2019, ambapo katika ziara hiyo atatembelea na kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo na kuongea na wananchi.

“Mheshimiwa Rais siku ya kwanza atapokelewa na viongozi wa serikali, chama pamoja na wananchi katika mpaka wa mkoa wa Njombe na mkoa wa Ruvuma na baada ya hapo atakwenda kuweka mawe ya msingi katika miradi mikubwa miwili, mradi wa kwanza itakuwa ni kuweka jiwe la msingi kwenye hospitali ya Rufaa ya mkoa, awamu ya kwanza imekamilika kwa upande wa huduma za wagonjwa wa Nje (OPD) na imegharimu kiasi cha Tshs. Bilioni 3.6”amesema Olesendeka.

Aidha, amesema kuwa ataweka jiwe la Msingi katika barabara ya Njombe-Moronga-Makete inayojengwa kwa kiwango cha lami kwa gharama ya takribani Tshs. Bilioni 217 ikiwa ni moja kati ya miradi ya barabara za lami na zege zinazojengwa mkoani Njombe yenye thamani ya zaidi ya Tshs. Bilioni 480 pamoja na kufanya mazungumzo na wananchi katika viwanja vya shule ya msingi Ramadhani.

Pia Rais Magufuli atafanya kazi ya kukaguwa miradi mikubwa miwili, mradi wa kwanza utakuwa ni wa kiwanda cha kabambe Tea factory unaomilikiwa na kampuni ya Uniliver Plc ya London nchini Uingereza kwa pamoja na kampuni ya Uniliver nv ya Roturdam nchini Netheland, pia atapata fursa ya kufungua mradi wa ujenzi wa barabara ya Mafinga-Makambako-Igawa eneo la mpaka wa Makambako na wilaya ya Wanging’ombe ambao ni kilometa 64.6 uliojengwa kwa kiwango cha lami ya kisasa na kugharimu Tshs. Bilioni 103,432,947,407.64 na baadaye atahutubia wananchi wa Makambako.

  • LIVE: Ziara ya Rais Magufuli mkoani Ruvuma 
  • Makonda atoa msaada wa milioni kumi kwa Wajane
  • Pierre amuibua Fatma Karume,’ Kila mtu ana haki ya kuishi atakavyo’

Hata hivyo, Ole Sendeka ametoa wito kwa wananchi wa mkoa wa Njombe na mikoa jirani ya Mbeya na Iringa kujitokeza kwa wingi katika maeneo ambayo miradi itazinduliwa pamoja na mikutano ya hadhara ili kumlaki na kumsikiliza Rais na kiongozi huyo wa kitaifa.

Aliyewatapeli mahujaji mwaka 2017 anusurika kichapo
Utoro watajwa kushusha kiwango cha ufaulu shule ya msingi Itulike mjini Njombe