Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kesho Julai 8, 2018 anatarajia kuipokea ndege mpya aina ya Boeing 787-8 Dreamliner ikitokea, Seattle nchini Marekani.

 Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Julai 7 na Kurugenzi ya mawasiliano Ikulu, ndege hiyo iliyonunuliwa na Serikali, inatarajiwa kutua Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere, saa 8 mchana.

Aidha, ndege hiyo ni ya nne kuwasili kati ya saba zilizonunuliwa na Serikali ya Tanzania kwa ajili ya kuliwezesha shirika la ndege la Tanzania (ATCL) ili kuimarsha huduma zake.

Video: Polepole ajibu kwanini CCM wanafanya mikutano, “Sisi tumekuwa wabunifu kwenye mbinu zetu”

Habari kubwa katika Magazeti ya Tanzania leo Julai 8, 2018
Video: Dkt. Mwigulu afunguka kuhusu kuacha ubunge, 'Nimerejea kwenye klabu yangu'

Comments

comments