Mwaka jana, Rais John Pombe Magufuli aliagiza kujengwa kwa ukuta utakaozunguka eneo la machimbo ya madini ya Tanzanite yanayopatikana Mererani, Kaskazini mwa Tanzania lengo likiwa kudhibiti wachimbaji wanaokwepa kulipa kodi na utoroshwaji wa madini hayo ambayo hupatikana Tanzania tu.

Hivyo kufuatia agizo hilo, leo Rais JPM anatarajia kuzindua ukuta huo wenye urefu wa kilomita 24.5 na urefu wa mita 3 kwenda juu, uliogharimu zaidi ya bilioni 6 za Kitanzania.

Aidha Rais Magufuli aliagiza ukuta huo uwe na kamera pamoja na mlango mmoja ambao utajengewa vifaa maalumu lemgo likiwa ni kudhibiti wizi unaofanywa na wachimbaji wadogo na wachimbaji wakubwa wa madini hayo ya Tanzanite.

‘’Waanze kujenga ukuta eneo hili lote na kazi hii ifanyike haraka, watakapojenga ukuta wataweka kamera na patakuwa na mlango mmoja ambao utajengewa vifaa maalumu, nataka niwaeleze ukweli ndugu zangu wa Simanjiro hata kama utameza Tanzanite itaonekana ‘’Magufuli.

Hata hivyo Februari mwaka huu, wakuu wa vyombo vya usalama, walitembelea eneo.

Wakitoa taarifa kwa viongozi wa ulinzi, wataalamu waliojenga ukuta huo, walisema licha ya kufanikisha ujenzi huo, changamoto mbalimbali walikutana nazo ikiwemo hatari inayo ukabili ukuta huo, kutokana na wachimbaji kulipua baruti, karibu na ukuta, hivyo kusababisha hatari za kuharibika haraka.

 

 

Zainab: Mke wa kwanza ni nafsi kitu pekee ambacho tutaondoka nacho duniani.
Video: Zitto Kabwe 'anunua kesi ya Nondo', Wabunge CCM na Chadema wachuana vikali bungeni

Comments

comments