Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli amesema ni marufuku kwa Jeshi lolote hapa nchini kuingia ubia na watu binafsi au kuuza maeneo yao kwaajili ya kufanyia biashara na kutaka maeneo yote ya Majeshi zibaki sehemu husika.

Ameyasema hayo jana baada ya kufanya ziara ya kushtukiza katika Gereza la ukonga lililoko jijini Dar es salaam, aidha katika hatua nyingine, Magufuli amepiga marufuku watu binafsi  kuuza sare za majeshi nchini na kuwataka wale wote wanaofanya hivyo kuzikabidhi mara moja kwa majeshi husika.

“Haiwezekani sare za majeshi yetu  hapa nchini kuuzwa na watu binafsi,haliwezekani kamwe labda baada ya kumaliza muda wangu”alisema Rais Magufuli.

Hata hivyo mbali na na maagizo hayo, Rais Magufuli ametoa  sh.10 bilioni kwa Jeshi la Magereza kwaajili ya kujenga nyumba mpya za makazi ya askari katika Gereza la Ukonga.

Magufuli amewahakikishia Maofisa askali Magereza kuwa Serikali itaendelea kuboresha maslahi yao na vitendea kazi kama inavyofanya kwa Majeshi mengine hapa nchini.

Andres Iniesta Aongeza Matumaini FC Barcelona
Mkaa wageuka dhahabu,Serikali kupandisha kodi